Godefrid Duynen
From Wikipedia, the free encyclopedia
Godefrid Duynen (1502 - 1572[1]) alikuwa padri mwanajimbo aliyefia imani ya Kikatoliki huko Uholanzi pamoja na wenzake 18 maarufu kama Wafiadini wa Gorkum[2].
Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu mfiadini. Kwanza alitangazwa na Papa Klement X kuwa mwenye heri tarehe 24 Novemba 1675, halafu mtakatifu na Papa Pius IX tarehe 29 Juni 1867.
Sikukuu yake na ya wenzake huadhimishwa tarehe ya kifodini chao, 9 Julai[3].