Gregori wa Utrecht
From Wikipedia, the free encyclopedia
Gregori wa Utrecht (Trier, leo nchini Ujerumani, 706 hivi – Utrecht, leo nchini Uholanzi, 776 hivi) alikuwa mmonaki maarufu kwa umisionari wake alioufanya tangu ujanani chini ya Bonifas mfiadini.
Ndiye aliyemweka kuwa abati wa kwanza wa Utrecht akafariki huko baada ya kuongoza jimbo hilo kwa niaba ya Papa bila kupewa daraja ya askofu[1].
Anaheshimiwa tangu zamani kama mtakatifu.