From Wikipedia, the free encyclopedia
Jokofu (pia: jirafu, tena friji kutoka neno la Kiingereza "fridge", kifupisho cha "refrigerator" kilichotumika tangu karne ya 17) ni chombo chenye umbo la kabati au sanduku kinachotumika mara nyingi kuhifadhi vinywaji, vyakula na vitu vingine kama hivyo ili viweze kudumu kwa muda mrefu zaidi ya siku zile ambazo zingedumu bila kuhifadhiwa humo. Ni aina za kipozaji kinachopoza yale yaliyo ndani yake.
Pia jokofu hutumika kwenye kugandisha vitu kama vinywaji, vyakula n.k. au hutumika kuvipa ubaridi.
Jokofu ni kifaa kilichotengenezwa na Wazungu kuanzia katikati ya karne ya 18, na hasa mwanzoni mwa karne ya 19.
Kabla ya uvumbuzi wa friji, barafu zilitumiwa kutoa hifadhi ya baridi kwa zaidi ya mwaka mzima. Njia ya asili bado hutumiwa wakati wa kula chakula cha leo. Kwenye milima au kwenye mchanga wa theluji ndiyo njia rahisi iliyotumiwa kufanya vinywaji kuwa baridi, na wakati wa majira ya baridi mtu anaweza kuweka maziwa safi kwa muda mrefu tu kwa kuiweka nje.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.