Judita Vannini
From Wikipedia, the free encyclopedia
Judita Vannini (7 Julai 1859 - 23 Februari 1911) alikuwa mwanamke wa Italia kaskazini ambaye, pamoja na Luigi Tezza, alianzisha shirika la Mabinti wa Mt. Kamili kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa.
Alitangazwa mwenye heri na Papa Yohane Paulo II tarehe 16 Oktoba 1994, halafu mtakatifu na Papa Fransisko tarehe 13 Oktoba 2019.
Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe ya kifo chake[1].