From Wikipedia, the free encyclopedia
Flavius Theodosius (11 Januari, 347 – 17 Januari, 395) alikuwa Kaizari wa Dola la Roma kuanzia 15 Mei, 392 hadi kifo chake.
Kabla hajatawala dola zima, alikuwa Kaizari upande wa Mashariki kuanzia Agosti 378. Upande wa Mashariki alimfuata Valens.
Theodosius alikuwa Kaizari wa mwisho aliyetawala dola zima la Roma. Ndiye aliyetangaza Ukristo wa Kikatoliki kuwa dini rasmi ya dola.
Hati ya Thesalonike ilisisitiza imani moja tu kuwa halali katika dola la Roma, ile "katholiki" (yaani, isiyo ya sehemu) na "orthodoksi" (yaani, sahihi).
Tangu hapo, Theodosius alitumia nguvu nyingi kuzima aina zote za Ukristo tofauti na hiyo, hasa Uario.[1]
Hati hiyo ilifuatwa mwaka 381 na Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli, uliothibitisha na kuongezea ungamo la Nisea katika Kanuni ya imani ya Nisea-Konstantinopoli.[2]
Mwaka 383, Kaisari alidai madhehebu mengine yote yampatie maungamo yao ya imani, akayachambua na kuyachoma yote isipokuwa ya Wanovasyani. Hivyo madhehebu hayo hayakuruhusiwa tena kukutana, kuweka mapadri wala kueneza mafundisho yao.[3] Theodosius alikataza wazushi wasiishi tena Konstantinopoli, na miaka 392-394 alitaifisha maabadi yao.[4]
Baada yake wanae wawili walishiriki utawala, Honorius upande wa Magharibi, na Arcadius upande wa Mashariki.
Waorthodoksi wanamheshimu kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 17 Januari.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.