Kana
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kana ya Galilaya (kwa Kigiriki: Κανὰ τῆς Γαλιλαίας) ni kijiji kinachotajwa mara kadhaa na Injili ya Yohane.
Humo tunasoma juu ya miujiza miwili ya Yesu:
- wa kwanza alipogeuza maji kuwa divai kwenye arusi ya Kana (2:1-11)[1].
- wa pili alipomponya mtoto wa diwani kutoka Kafarnaumu (4:46 n.k.).
Pia kinatajwa kama asili ya Nathanaeli (21:2)[2].