![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/0/0d/Kangaroo_and_joey03.jpg/640px-Kangaroo_and_joey03.jpg&w=640&q=50)
Kangaruu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kangaruu (kutoka Kiingereza: kangaroo) ni jina la wanyama mamalia wa spishi mbalimbali walio wenyeji wa Australia. Wote ni wala majani wanaobeba watoto wao wachanga ndani ya pochi ya ngozi iliyopo nje ya mwili juu ya tumbo wakiwa spishi zinazojulikana zaidi ya wanyama wa ngeli ndogo ya marsupialia. Familia ya spishi zao huitwa kwa jina la biolojia Macropodidae yaani wenye miguu mikubwa (kwa Kigiriki makrós (kubwa) na poús (mguu)). Familia hiyo ina spishi takriban 60.
Kangaruu | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Jike la kangaruu kijivu mashariki (Macropus fuliginosus) akiwa na ndama wake kwenye pochi | ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Spishi 4:
| ||||||||||||||||
Kwa matumizi ya kawaida neno hili hutumika kuelezea spishi hii kutoka kwenye familia kubwa hasa wale wa jenasi ya Macropus, kangaruu mwekundu, kangaruu wa kijivu wa magharibi na kangaruu wa kijivu wa mashariki [1]. Kangaruu ni wazawa wa bara la Australia. Jamii nyingine kangaruu wengine wanapatikana pia Australia na New Guinea.
Kangaruu wakubwa wamezoea mabadiliko yaliyosababishwa na kilimo cha kibinadamu katika mazingira yao asilia lakini wale wa spishi za wadogo wengi wapo hatarini. Hawafugwi kwa lolote lakini kangaruu wa mwituni wanawindwa kwa ajili ya nyama, michezo na kulinda malisho ya kondoo na ng'ombe [2] japo kwa vipingamizi. Uwindaji wa kangaroo una faida kubwa kimazingira na kiafya kwa ngombe na kondoo wanaochungwa kwa ajili ya nyama.[3]
Kangaroo ni alama ya taifa ya Australia picha yake inatumika katika ngao ya taifa , kwenye pesa zake na baadhi ya mashirika makubwa ya Australia. Kangaroo ni muhimu sana kwa utamaduni na sura ya taifa ya Australia.