Kasiani wa Imola
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kasiani wa Imola (alifariki Forum Cornelii, leo Imola, Italia, karne ya 4) alikuwa mwalimu huko Imola, leo katika mkoa wa Emilia-Romagna huko Italia kaskazini) aliyekuwa akifundisha pia imani ya Kikristo.
Aliposhtakiwa alikataa kukana imani hiyo ili kuabudu miungu, akaadhibiwa kwa kumfanya auawe na wanafunzi wake kwa kalamu zao [1][2]; hivyo, kadiri mkono ulivyokuwa dhaifu, mateso yalikuwa makali zaidi.
Tangu zamani anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.