Kiki Camarena
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kwa kihispania, sehemu ya kwanza la jina lake ni Camarena na jina la pili na la kuzaliwa Salazar.
Enrique "Kiki" Camarena Salazar (Julai 26, 1947 - Februari 9, 1985), alikua afisa intelegensia wa Marekani kwenye shikirika la kuzuia ulanguzi wa madawa ya kulevya (DEA). Mnamo Februari mwaka 1985 alitekwa nyara na walanguzi madawa ya kulevya walioajiriwa na wanasiasa wa Mexico huko Guadalajara, Mexico. Alihojiwa kwa kuteswa na mwisho kuuwawa. Viongozi watatu wa Karume ya Guadalajara hatimae kuhukumiwa kwa mauaji ya Camarena huko Mexico. [1]
Uchunguzi wa Marekani kwenye mauaji ya Camarena yalipelekea kwa kesi zingine kumi huko Los Angeles kwa watu wa taifa la Mexico waliohusika na uhalifu huo. Muendelezo wa kesi hio ulitatiza mahusiano baina ya Marekani na Mexico (U.S.-Mexican Relation), hasa hasa pale mmoja wa watuhumiwa, Rafael Caro Quintero aliachiliwa kutoka jera mnamo 2013. Caro Quintero alishikiliwa tena na vikosi vya Mexico mnamo Julai 2022.[1][2]