Kundi la majarra
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kundi la majarra (kwa Kiingereza: galaxy group) ni idadi ya majarra zinazoshikamana katika anga-nje. Maana zinaathiriana kwa njia ya mvutano wake. Katika mpangilio huo ni hadi majarra 50 zinazotazamwa kuwa kundi.
Kama idadi ya majarra zinazoshikamana ni kubwa zaidi jumla yake ni fundo la majarra.
Majarra za kundi moja zinaenea katika nafasi yenye kipenyo cha takriban miakanuru milioni 10 hivi; masi ya majarra zote kwa pamoja ndani ya kundi ni hadi masi za Jua 1013.[1]
Majarra yetu ya Njia Nyeupe ni sehemu ya kundi janibu la majarra pamoja na majarra 40 hivi nyingine.[2] Pamoja na Njia Nyeupe kuna Majarra ya Mara (inaitwa pia M31) katika kundinyota Mara, ya M33 katika Pembetatu na majarra ndogo kama Mawingu ya Magellan.