Ludmila
From Wikipedia, the free encyclopedia
Ludmila (Melnik[1] , 860 hivi - Tetin, 15 Septemba 921) alikuwa mke wa mtawala (kníže) wa Bohemia na bibi tena mlezi wa Wenseslaus I[2] aliyejitahidi kumfanya ampende Yesu na Ukristo aliouongokea mwenyewe na mume wake kwa juhudi za Methodio[2][3].
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/b/b7/StLudmilaWindowCedarRapidsSep2001.jpg)
Alinyongwa kwa njama ya mkwe wake na masharifu kadhaa[2][4].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini[3].
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 16 Septemba[5].