Orodha ya Marais wa Urusi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Ukarasa huu una orodha ya Marais wa Urusi au Shirikisho la Urusi (kwa Kirusi: Президент России) tangu mwaka 1991. Kabla ya hapo nchi ilikuwa na katiba tofauti ikiitwa Shirikisho la Jamhuri ya Kisovyiet ya Kijamii ya Kirusi na hapo Kamati ya Kudumu ya Utendaji ya Sovyeti Kuu ilikuwa na nafasi inayolingana na uraisi; mara nyingi mwenyekiti wa kamati ya kuduma alitajwa kuwa kama "rais". Kabla ya mapinduzi ya 2017 mkuu wa dola alikuwa kaizari au tsar wa Urusi.