Maria Nyerere
From Wikipedia, the free encyclopedia
Maria Nyerere (alizaliwa kama Maria Waningu Gabriel Magige[1] mnamo 31 Disemba 1930[2][3]) alikuwa mke wa rais wa kwanza wa Tanzania Mwl Julius Kambarage Nyerere kuanzia 1964 hadi 1985.[4] Kwa kawaida nchini Tanzania anajulikana kama 'Mama Maria' tu.[5][6]
Maria Nyerere | |
Maria (kulia) na Evelyn Macleod | |
Mke wa rais wa kwanza wa Tanzania | |
Muda wa Utawala 29 Oktoba 1964 ā 5 Novemba 1985 | |
mtangulizi | Mwanzilishi |
---|---|
aliyemfuata | Siti Mwinyi |
Mke wa rais wa Tanganyika | |
Muda wa Utawala 9 Disemba 1962 ā 25 Aprili 1964 | |
tarehe ya kuzaliwa | 31 Desemba 1930 (1930-12-31) (umri 93) Tanganyika |
utaifa | Mtanzania |
chama | Chama Cha Mapinduzi |
ndoa | Julius Nyerere (1953-1999) |
watoto | 7
|
mhitimu wa | Sumve Teacher Training College |
Fani yake | Mwalimu |
dini | Mkristo - Katoliki |
Alikuwa mtoto wa saba kati ya tisa wa Gabriel Magige, wa Baraki, Tareme[7], kutoka kwa mkewe Hannah Nyashiboha.[8]
Maria alisoma katika shule "White Sisters' School" iliyokuwa Nyegina, kisha shule ya Ukerewe, kisha akajiunga na chuo cha ualimu "Sumve Teacher Training College"; alihitimu kwa kupata cheti cha ualimu akaanza kufundisha katika Shule ya Msingi Nyegina iliyoko Musoma.[9] Aliolewa na Julius Nyerere mwaka 1953.
Kwa sasa ni miongoni mwa wajumbe saba wa baraza la wazee wa "Alliance for Tanzania Youth Economic Empowerment" (Atyee), pamoja na rais wa zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi na rais wa zamani wa Zanzibar Amani Abeid Karume ambaye alikuwa mtoto wa Rais wa kwanza wa Zanzibar.[10]