Martin de Porres
From Wikipedia, the free encyclopedia
Martin de Porres (1579 – 3 Novemba 1639) alikuwa bradha wa Shirika la Wahubiri katika nchi ya Peru.
Akiwa mtoto chotara wa kabaila Mhispania Juan de Porres na binti mwenye asili ya Afrika Anna Velasquez hakutambuliwa na baba yake akalelewa na mama na kuwa msaidizi wa daktari akijifunza hivyo elimu ya matibabu.
Mwaka 1594 alijiunga na watawa Wadominiko akaendelea kuwaangalia wagonjwa wa matabaka na rangi zote.
Alikuwa na kipaji cha uponyaji ambacho kiliwasaida watu wengi. Kutokana na upendo aliowaonyesha watu wote aliheshimiwa sana na taarifa za uponyaji wa ajabu zilianza kuenea.
Mwaka 1837 alitangazwa mwenye heri na Papa Gregori XVI, halafu tarehe 6 Mei 1962 akatangazwa na Papa Yohane XXIII kuwa mtakatifu.