![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/d/d0/Periodic_waves_in_shallow_water.png/640px-Periodic_waves_in_shallow_water.png&w=640&q=50)
Masafa ya mawimbi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Masafa ya mawimbi (pia urefu wa wimbi[1], mara chache lukoka[2]; kwa Kiingereza wavelength) ni namna ya kupima na kutaja ukubwa wa wimbi.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/d/d0/Periodic_waves_in_shallow_water.png/640px-Periodic_waves_in_shallow_water.png)
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/6/62/Sine_wavelength.svg/320px-Sine_wavelength.svg.png)
Ni umbali kati ya sehemu za kulingana za mawimbi mawili ambayo yanafuatana, kwa mfano kati ya kilele na kilele au mabonde yao.
Mawimbi yapo kila sehemu ya mazingira asilia, kwa mfano:
- mawimbi ya maji
- mawimbisauti
- mawimbi sumakuumeme pamoja na nuru na wimbiredio
Masafa ya mawimbi hutofautiana sana. Mawimbi marefu yanayoweza kutambuliwa na milango ya fahamu ya binadamu ni sauti ya besi yenye masafa ya mita 21. Sikio letu linatambua mawimbi yenye masafa kati ya milimita 17 hadi mita 21.
Mawimbi sumakuumeme yana upeo mkubwa.
- Masafa ya wimbiredio ni kati ya milimita 1 hadi kilomita 100.
- nuru inayoonekana kwa macho yetu ina masafa kati ya nanomita 380 (urujuani) hadi 780 (nyekundu). Nyuki huona pia mnururisho mfupi zaidi yaani urujuanimno, lakini hawaoni nyekundu.
- eksirei zina masafa baina ya nanomita 0.01 hadi 10.
- masafa ya mawimbi gammarei iko katika upeo wa pikomita.