Elisha
From Wikipedia, the free encyclopedia
Elisha (kwa Kiebrania אֱלִישַׁע, Elisha, yaani "Mungu wangu ni wokovu", kwa Kigiriki Ἐλισσαῖος, Elissaios au Ἐλισαιέ, Elisaie, kwa Kiarabu الْيَسَع Elyasaʿ) alikuwa nabii anayetajwa katika Biblia na katika Qur'an.
Mwanafunzi wa Elia, ingawa hakuacha maandishi, alitabiri wokovu ujao wa mataifa yote kwa miujiza aliyowafanyia watu wasio Waisraeli[1].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.