Nguchiro
From Wikipedia, the free encyclopedia
Nguchiro (Kiing. mongoose) ni wanyama wadogo kiasi wa familia Herpestidae. Kuna spishi nne huko Madagaska ziitwazo nguchiro pia (nguchiro-bukini) na ambazo ziliainishwa katika Herpestidae, lakini malinganisho ya ADN yameonyesha kwamba spishi hizi zina mnasaba zaidi na spishi za Eupleridae. Sasa zimepewa nusufamilia yao binafsi Galidiinae. Nguchiro wa kweli wanatokea Afrika, Asia na Ulaya ya kusini. Wamewasilishwa katika visiwa kadhaa vya Karibi na Hawaii ambapo wamekuwa usumbufu.
Nguchiro | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Nguchiro mwembamba (Galerella sanguinea) | ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Jenasi 13:
| ||||||||||||
Usambazaji wa nguchiro (kuna spishi zaidi ambapo rangi ni nzito zaidi) | ||||||||||||
Wanyama hawa ni warefu na wembamba na wana mkia mrefu wenye manyoya mengi. Wanafanana na chororo lakini wako wakubwa zaidi. Rangi yao ni hudhurungi, kahawia, kijivu au nyeusi. Wao ni wanyama mbua na hula wadudu, kaa, nyungunyungu, mijusi, nyoka, ndege na wagugunaji, na mara nyingi mayai na mizoga pia. Nguchiro hujulikana kwa uwezo wao wa kuua nyoka na kukinga sumu yao. Huishi peke yao au kwa makundi (k.m. nguchiro miraba na nguchiro-jangwa) na hukiakia mchana lakini pengine usiku pia.