Nilo wa Sinai
From Wikipedia, the free encyclopedia
Nilo wa Sinai (pia: Nilo wa Ankara, Nilo Mzee; karne ya 4 – 430 hivi) anafikiriwa kuwa mfuasi wa Yohane Krisostomo[1].
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/4/4f/Nil_Postnik.jpg/220px-Nil_Postnik.jpg)
Baada ya kuwa meya wa jiji la Konstantinopoli, alikwenda kuishi kama mmonaki kwenye Mlima Sinai pamoja na mtoto wake Theodulo, huku mke wake na mtoto mwingine wakienda kuishi vilevile nchini Misri.
Mwishoni[2] akawa abati wa monasteri karibu na Ankara, Galatia, leo nchini Uturuki[3], maarufu pia kwa maandishi yake[4][5].
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake ni tarehe 12 Novemba[6].