Nyanda za Juu za Mongolia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Nyanda za Juu za Mongolia ni sehemu za Nyanda za Juu za Asia ya Kati zinazoenea katika Mongolia na kaskazini mwa China kwa takriban kilomita za mraba 3,200,000. Inapakana na Milima ya Hinggan Kubwa upande wa mashariki, Milima ya Yin upande wa kusini, milima ya Altai upande wa magharibi, na milima ya Sayan na Khentii upande wa kaskazini. [1]
Ndani ya nyanda za juu liko Jangwa la Gobi na pia maeneo makubwa ya nyika kavu. Mwinuko uko takriban mita 1,000 hadi 1,500 juu ya u.b.
Kisiasa, eneo lote limegawanywa kati ya Mongolia, China na Urusi. Upande wa China, sehemu za Mongolia ya Kichina na mkoa wa Xinjiang ni sehemu ya nyanda za juu za Mongolia. Huko Urusi, ni sehemu za Buryatia na kusini mwa Irkutsk Oblast.