Paulo Chen Changpin
From Wikipedia, the free encyclopedia
Paulo Chen Changpin (1838 hivi - Qingyan 29 Julai 1861) alikuwa mseminari wa China aliyefia Ukristo pamoja na Yosefu Zhang Wenlan, Yohane Mbatizaji Luo Tingyin na Martha Wang Luoshi.
Walifungwa katika handaki lenye joto na unyevu mwingi, waliteswa kikatili na hatimaye walikatwa kichwa[1].
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu pamoja na wengine 119 tarehe 1 Oktoba 2000.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 9 Julai, lakini ya kwake mwenyewe tarehe ya kifodini chake[2].