Saola
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Saola | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Saola (Pseudoryx nghetinhensis) | ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Msambao wa saola | ||||||||||||||||||
Saola ni mnyama wa pori wa spishi Pseudoryx nghetinhensis katika familia Bovidae, aliye mmoja wa mamalia adimu zaidi kuliko wote duniani. Huyo ndiye mnyama pekee katika jenasi Pseudoryx.
Saola huishi misitu ya Vietnam na Laos. Saola ana mnasaba na ng'ombe, nyati na baisani,[1] na spishi hiyo iliainishwa baada ya mzoga wake umegunduliwa na kikosi cha pamoja cha Wizara ya Misitu na "WWF", mnamo 1992 katika Hifadhi ya Vũ Quang, Vietnam.[2] Kikosi hicho kiliona fuvu tatu za kichwa zenye pembe nyofu ndefu zisizo za kawaida, zilizowekwa nyumbani mwa wawindaji. Katika makala yao, kikosi kilipendekeza kufanywa "uchunguzi wa miezi mitatu kuangalia mnyama hai", lakini tupo miaka 20 baadaye, na bado hakuna mwanasayansi yeyote ambaye amemwona saola porini. Lakini saola hai alipigwa picha porini, mnamo Septemba ya 2013, na mtego wa kamera. Van Ngoc Thinh, mkurugenzi wa taifa wa WWF Vietnam, alisema "Huu ni ugunduzi muhimu na umetoa tena matumaini kwa ajili ya kufufua kwa spishi hiyo."[3][4] Idadi ya Saola wanaoishi haijuliwi, kama wanyama 11 tu wamerekodiwa wakiwa hai.
Mnamo mwisho wa Agosti 2010, saola mmoja alikamatwa na wanakijiji Laos, lakini alikufa wakati alipokuwepo hali ya kufungwa, kabla ya wanahifadhi wa serikali hawajapanga kumwacha saoga kurudi porini. Mzoga unachunguzwa kuboresha ujuzi wa kisayansi wa saola.[5][6] Mara nyingine, wanyama hao wategwa katika mitego ambayo imewekwa kushika wanyama kama nguruwe mwitu wajao kula mimea ambayo imepandwa na wakulima. Zaidi ya mitego 26,651 imeondolewa kutoka makazi ambapo saola ameishi kwa miaka mingi.[7]
Hadi sasa, saola wote ambao wamekamatwa wamekufa; hayo yamesababisha mawazo kwamba spishi hiyo haiwezi kuishi kwa kufungwa.