Serafino wa Montegranaro
From Wikipedia, the free encyclopedia
Serafino wa Montegranaro (1540 – 12 Oktoba 1604), alikuwa bradha wa shirika la Ndugu Wadogo Wakapuchini kutoka Italia ya Kati.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/f/f7/San_Serafino_de_Montegranaro.jpg/220px-San_Serafino_de_Montegranaro.jpg)
Bradha asiye na vipawa vingi kiutu bali mwenye karama za ajabu, anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu tangu alipotangazwa na Papa Klementi XIII tarehe 16 Julai 1767.