Shilo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Shilo ulikuwa mji wa zamani unaotajwa katika Biblia ya Kiebrania, karibu na Khirbet Seilun, kusini kwa Tirza.[1]
Ulikuwa makao ya hekalu lilipotunzwa sanduku la agano kabla ya hilo kutekwa na Wafilisti wakati wa kuhani Eli na hatimaye kuhamishiwa na mfalme Daudi mjini Yerusalemu, ambapo mwanae Solomoni alilijengea hekalu la fahari.
Nabii Yeremia alichukua Shilo kama kielelezo cha maangamizi yatakayolipata hekalu la Yerusalemu kutokana na Waisraeli kutokubali ujumbe wa toba aliowaletea kutoka kwa Mungu.