Sidoni
From Wikipedia, the free encyclopedia
Sidoni (kwa Kiarabu صيد, Ṣaydā, kwa Kigiriki Σιδών, Sidon) ni mji wa Lebanoni kusini, katikati ya Beirut na Tiro, maarufu katika historia ya kale hasa kwa utajiri uliotokana na biashara yake ya kupitia baharini. Hata leo unategemea sana bandari yake, mbali ya utalii.
Wakazi walikuwa 65,000 hivi mwaka 2000, lakini pamoja na eneo la kandokando wanafikia 200,000[1][2] na kuufanya mji wa tatu nchini Lebanoni.