Sao Tome
From Wikipedia, the free encyclopedia
Sao Tome ni mji mkuu wa nchi ya visiwa ya Sao Tome na Principe, karibu na Afrika ya Magharibi.
Jina limetokana na lile la Kireno la Mtakatifu Thoma.
Mji ulianzishwa na Ureno mwaka 1485 kwenye pwani ya kaskazini-mashariki ya kisiwa chenye jina lilelile katika ghuba ya Guinea.
Mji ulikuwa na wakazi 56,166 mwaka 2005.
Kuna kiwanja cha ndege cha kimataifa na viwanda kadhaa ya matofali, sabuni na vinywaji.
Sao Tome ina shule za msingi hadi sekondari, makanisa, hospitali ya pekee nchini, vituo vya TV na redio.