Tambarare ya Ulaya ya Mashariki
From Wikipedia, the free encyclopedia
Tambarare ya Ulaya ya Mashariki inaenea katika Ulaya ya Mashariki, hasa katika Urusi. [1] Inaanza takribani kwenye longitudo ya nyuzi 26 ikielekea upande wa mashariki.
Tambarare hiyo inajumuisha mabeseni ya mito Dnepr, Oka, Don na Volga. Upande wa kusini mpaka uko kwenye safu za milima za Kaukazi na Krimea[2].
Upande wa magharibi inaendelea katika Tambarare ya Ulaya Kaskazini ilhali zote ni sehemu za Tambarare ya Ulaya (European Plain) katika Uholanzi, Ujerumani hadi kaskazini-mashariki mwa Poland). Ndiyo sehemu kubwa ya Ulaya isiyo na milima. [3]
Nyanda za chini za Ulaya Mashariki zinajumuisha nchi za Kibalti, Belarusi, Ukraine, Moldova, Romania na sehemu ya Ulaya ya Urusi.
Eneo lote ni takriban kilometa mraba milioni 4 likiwa kwa wastani mita 170 juu ya UB.