Tibursi, Valeriani na Masimo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Tibursi, Valeriani na Masimo (walifariki mjini Roma, Italia, 229) walikuwa wanaume walioongokea Ukristo. Kwa sababu hiyo waliteswa na kuuawa wakati wa dhuluma ya Dola la Roma dhidi ya Wakristo, chini ya kaisari Alexander Severus[1].
Inasemekana Valeriani alikuwa mume wa Sesilia ambaye alimvuta katika Ukristo, naye akamvuta ndugu yake, Tibursi. Walipokamatwa, afisa Masimo aliamua kuwafuata akauawa siku chache baadaye[2].
Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.