![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/2/26/Mbombela_Stadium_arena.jpg/640px-Mbombela_Stadium_arena.jpg&w=640&q=50)
Uwanja wa michezo wa Mbombela
From Wikipedia, the free encyclopedia
Uwanja wa michezo wa Mbombela ni uwanja wa michezo wa shirikisho la mpira wa miguu na umoja wa michezo ya raga(rugby) unaopatikana Mbombela, hapo zamani palifahamika kama Nelspruit katika jimbo la Mpumalanga, Afrika Kusini. Ulijengwa kwa ajili ya kombe la Dunia la FIFA la mwaka 2010. Ni moja wapo ya viwanja 10 vilivyotumika kwa michezo ya soka na moja kati ya viwanja 5 vipya vilivyo jengwa kwa ajili ya kombe la dunia la mwaka 2010. Ni uwanja wa nyumbani kwa klabu ya Pumas na unauwezo wa kubeba washabiki 40,929 na wote wakiketi kwenye viti.[1]
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/2/26/Mbombela_Stadium_arena.jpg/640px-Mbombela_Stadium_arena.jpg)
Unapatikana kilomita sita(6) magharibi mwa jimbo la Mpumalanga na ndio uwanja mkubwa kuliko vyote katika hilo jimbo. Kiasi cha R1,050-milioni kilitumika kujenga uwanja huu na uwanja ulikuwa tayari kabla ya Juni 2010 na fedha zote zilitolewa na serikali kuu kupitia mapato ya ushuru na hapakuwa na kiasi chochote cha fedha kilichohitajika kutoka halmashauri ya jiji.