Uwanja wa michezo uliopo Soweto, Afrika Kusini From Wikipedia, the free encyclopedia
Uwanja wa michezo wa Orlando ni uwanja unaotumika kwa michezo mbalimbali huko Soweto kitongoji cha Johannesburg kilichopo Gauteng nchini Afrika Kusini. Ni uwanja wa nyumbani wa klabu ya mpira wa miguu ijulikanayo kwa jina la {Orlando Pirates}, timu mashuhuri ya soka ambayo hucheza katika Ligi kuu ya soka ya {Afrika Kusini}.[1] [2] [3]
Uwanja huu hapo awali ulijengwa na Chama cha soka cha {Johannesburg Bantu} ambapo ulikuwa na uwezo wa kukaa watu wapatao elfu ishirini na nne (24,000) ambapo matengenezo yaligharimu kiasi cha £37,500. Ulifunguliwa na Waziri wa maendeleo ya Bantu, MC de Wet Nel na (Ian Maltz) ambaye kwa wakati huo alikuwa Meya wa Johannesburg mnamo tarehe 2 Mei 1959.[4][5]
Mnamo mwaka 1978, timu ya Soka ya Orlando ilimchukua (Phil Venter) ambaye alikuwa mchezaji mweupe wa kwanza wa Shirikisho la soka Kitaifa kuichezea timu ya watu weusi. Badae alijiunga na mchezaji mwingine mweupe aitwaye (Keith Broad).[6]
Mnamo mwaka 1995, Uwanja huo ulikuwa mwenyeji katika mazishi ya Kigogo wa African National Congress ajulikanaye kama Joe Slovo, na pia yale ya Walter Sisulu yaliyotokea mnamo mwaka 2003 ambapo Thabo Mbeki, Nelson Mandella, Joaquim Chissano wa Mozambique, Robert Mugabe wa Zimbabwe, na Pakalitha Mosisili wa Lesotho alikuwa miongoni mwa waombolezaji walioshiriki.[7] [8]
Mnamo mwaka 2011, uwanja huo pia uliandaa mazishi ya Albertina Sisulu ambapo Jacob Zuma, Jakaya Kikwete wa Tanzania na Kenneth Kaunda wa Zambia walikuwa miongoni mwa waombolezaji, pia katika mazishi ya Winnie Mandela mnamo mwaka 2018 ambapo Cyril Ramaphosa, Raisi wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki, Kgalema Motlanthe, Jacob Zuma, Hage Geingob wa Namibia, Denis Sassou Nguesso wa Kongo-Brazaville na Mokgweetsi Masisi wa Botswana na Naomi Campbell wa (Britain) walikuwa kati ya waombolezaji walioshiriki.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.