Vijili wa Salzburg
From Wikipedia, the free encyclopedia
Vijili wa Salzburg (kwa Kilatini Vergilius, kwa Kigaelic Feirgil, 700 hivi - 27 Novemba 784) alikuwa mmonaki na mwanaastronomia kutoka Eire.
Mnamo mwaka 743 alihamia Ufaransa, ambapo alipokewa na mfalme Pipino Mfupi.
Baada ya kuishi miaka miwili huko Cressy, karibu na Compiègne, alikwenda Bavaria, kwa mwaliko wa mtemi Odiloni wa Bavaria, aliyemfanya askofu wa Salzburg (leo nchini Austria) mwaka 748.
Alijitahidi sana kueneza Ukristo kati ya wananchi wa Karinthia.
Alitangazwa mtakatifu na papa Gregori IX mwaka 1233.