Yefta
From Wikipedia, the free encyclopedia
Yefta (kwa Kiebrania יפתח, Yip̄tāḥ) alikuwa mmojawapo kati ya Waamuzi wa Biblia.
Kadiri ya Waamuzi 11-12 alikuwa wa kabila la Manase au wa kabila la Gadi akaongoza Israeli kwa miaka 6[1].
Alikuwa na mtoto mmoja tu, tena wa kike[2], lakini alimtoa sadaka kwa Mungu kama shukrani kwa kumpa ushindi vitani dhidi ya Waamoni. Alifanya hivyo ili kutimiza nadhiri aliyoweka kwanza, bila kujua kwamba Torati inakataza sadaka za namna hiyo.