Yohane Gabrieli Perboyre
From Wikipedia, the free encyclopedia
Yohane Gabrieli Perboyre, C.M. (Montgesty, Lot, 6 Januari 1802 – Wuchang, Hubei, 11 Septemba 1840) alikuwa padri wa shirika la Vinsenti kutoka Ufaransa aliyefanya umisionari nchini China.
Katika kuhubiri Injili alijilinganisha na desturi za wananchi, lakini dhuluma ilipolipuka aliteswa kwa namna mbalimbali wakati wa kufungwa kwa muda mrefu akauawa huko msalabani kwa ajili ya imani yake ya Kikristo[1].
Alitangazwa mwenye heri na Papa Leo XIII tarehe 10 Novemba 1889, halafu mtakatifu na Papa Yohane Paulo II tarehe 2 Juni 1996[2].