Yosefu Sebastiani Pelczar
From Wikipedia, the free encyclopedia
Yosefu Sebastiani Pelczar (17 Januari 1842 – 28 Machi 1924) alikuwa askofu wa Przemyśl (leo nchini Polandi) kuanzia mwaka 1900 hadi kifo chake.[1]
Pamoja na kuwa mwalimu maarufu wa maisha ya Kiroho, alisaidia watu kwa kila namna na kuanzisha shirika la Wajakazi wa Moyo Mtakatifu wa Yesu[2].
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 2 Juni 1991 halafu mtakatifu tarehe 18 Mei 2003.[3]