Yosefu wa Arimataya
From Wikipedia, the free encyclopedia
Yosefu wa Arimataya alikuwa Myahudi mwanamume wa karne ya 1, maarufu hasa kutokana na habari zake zinazopatikana katika Injili (Mk 15:42-46; Math 27:57-60; Lk 23:50-53; Yoh 19;38-42).
Habari za ziada, lakini si za kuaminika, zinapatikana katika vitabu ambavyo havimo katika Biblia ya Kikristo, hasa Injili ya Nikodemu.
Tajiri na mtu wa baraza la Israeli, aliyetarajia Ufalme wa Mungu uliotangazwa na Yesu, alichukua jukumu la kumzika, akiomba ruhusa ya Ponsyo Pilato na kujitolea kaburi alilokuwa amejiandalia pangoni kwenye Kalivari[1].
Anaheshimiwa kama mtakatifu na Kanisa Katoliki, Waorthodoksi, Waanglikana, Walutheri na madhehebu mengine ya Ukristo.