ARPANET
ulikuwa ndio mfumo wa kwanza wa intaneti kutumika, na mfumo wa kwanza kutumia TCP/IP protokali za kimuunganiko baina ya vifaa viwili vya kielektroniki. From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Advanced Research Projects Agency Network (kifupi: ARPANET) ulikuwa ndio mfumo wa kwanza wa intaneti kutumika, na mfumo wa kwanza kutumia TCP/IP protokali za kimuunganiko baina ya vifaa viwili vya kielektroniki. Misemo yote hii ndiyo inayotumika kiufundi katika kuielezea intaneti.


ARPANET ilianzishwa na Advanced Research Projects Agency (ARPA) ya huko nchini Marekani inayojihusisha na mambo ya kiusalama ya nchi hiyo.[1]
Katika harakati za kuendeleza mawazo ya J. C. R. Licklider , Bob Taylor ndiyo yaliyopelekea kuzinduliwa kwa mradi huu wa ARPANET mnamo mwaka 1966 na kuwezesha kompyuta mbalimbali kuwasiliana.[2] Taylor alimteuwa Larry Roberts kama msimamizi wa programu . Roberts ndiye alikuwa akitoa mbinu na namna ya kuunda mifumo ya kimtandao.[3] Alijaribu kuzitumia mbinu za Donald Davies’ katika kupelekea kufanyika uzinduzi wa ubadilishaji wa pakiti ,[4] na alitumia mbinu za uingizaji kutoka kwa Paul Baran.[5] ARPA ilimpa mkataba wa utengenezwaji wa mfumo wa mtandao kwa Bolt Beranek & Newman ambaye alikuja kutengeneza,kwa mara ya kwanza protokali ya mawasiliano kwenye mitandao .[6] Roberts alimhusisha Leonard Kleinrock kutoka Chuo Kikuu Cha Carlifonia katika kuunda mfumo wa kimahesabu wa kuorodhesha teknolojia ya mtandao wa pakiti.[5]
Kompyuta za mara ya kwanza kabisa kuunganishwa,ziliunganishwa mnamo mwaka 1969 na programu ya kudhibiti mtandao na hivyo kuanza kufanya kazi rasmi mnamo 1970 .[7][8] Uzinduzi na maendeleo ya programu ulipelekea Utawala wa mbali, uhamisho wa faili na barua pepe.[9] Mfumo huu ulianza kukuwa kwa haraka sana na hivyo kutajwa kuwa unafanya kazi vizuri 1975 pindi kampuni hiyo ya udhibiti kuipitsha kwa shirika la masuala ya kiulinzi lijulikanalo kama shirika la mawasiliano ya ulinzi.
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads