Abiya

From Wikipedia, the free encyclopedia

Abiya
Remove ads

Mfalme Abiya (kwa Kiebrania: אֲבִיָּם, ʼAvīyam au ʼĂḇīyyām; yaani "Baba wa bahari" au "Baba yangu ni bahari"; pia: אֲבִיָּה, ʼAbiyya, "Baba yangu ni YHWH"; 950 KK hivi - 911 KK) alitawala ufalme wa Yuda kati ya miaka 913 KK na 911 KK.

Thumb
Mfalme Abiya alivyochorwa na Guillaume Rouillé mwaka 1553.

Muda huo alijitahidi kurudisha chini ya ukoo wake makabila yote ya Israeli yaliomuasi baba yake, Rehoboamu, mwana wa Solomoni.

Alikuwa na wake 14, watoto wa kiume 22 na wa kike 16.

Habari zake zinapatikana hasa katika Kitabu cha Pili cha Wafalme 15 na Kitabu cha Pili cha Mambo ya Nyakati 12-13.

Pia anatajwa na Injili ya Mathayo kati ya mababu wa Yesu Kristo.

Remove ads

Tanbihi

Marejeo

Marejeo mengine

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads