Rehoboamu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Rehoboamu (kwa Kiebrania: רְחַבְעָם, Rəẖavʻam au Reḥaḇʻām; kwa Kigiriki: Ροβοαμ, Rovoam; kwa Kilatini: Roboam; 970 KK-910 KK hivi) alikuwa mfalme wa nne wa Israeli.


Habari zake zinapatikana katika Biblia (Kitabu cha Kwanza cha Wafalme na kitabu cha Pili cha Mambo ya Nyakati).
Alikuwa mtoto na mrithi wa Solomoni[1], lakini alisababisha uasi wa makabila ya kaskazini yakiongozwa na Yeroboamu I, akajikuta amebaki na yale ya kusini tu.
Kadiri ya Kitabu cha Kwanza cha Wafalme (12:22-24) na Kitabu cha Pili cha Mambo ya Nyakati (11:2-4; 12:5-7) nabii Shemaya alimzuia Rehoboamu asipigane vita na Yeroboamu I ili kujirudishia mamlaka juu ya makabila hayo yaliyoasi[2].
Pia alimtabiria adhabu ya Mungu kumpitia farao Shishak wa Misri kwa makosa yake.
Mama wa Rehoboamu alikuwa si Mwisraeli, bali Mwamoni. Mwenyewe alioa wake 18 na masuria 60 na kupata watoto 88: 28 wa kiume na 60 wa kike.
Rehoboamu alitawala miaka 17 akarithiwa na mwanae Abiya.
Remove ads
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads