Akiles
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Akilesi (pia: Akile, Kigiriki: Ἀχιλλεύς, Akhilleus ) alikuwa shujaa wa mitholojia ya Kigiriki aliyepigania Vita ya Troia na ndiye mhusika mkuu katika Iliadi ya Homeri.

Alitajwa kuwa mwana wa shujaa Peleo na nereidi Thetisi. Katika shairi ya Homeri anaingia kama kiongozi wa kabila la Ugiriki ya Kaskazini, akipita mashujaa wote kwa nguvu na uwezo.
Masimulizi ya Shairi ya Iliadi yanaanza kwa taarifa ya mabishano baina Akilesi na mfalme Agamemnon, aliyekuwa mkuu wa jeshi la Wagiriki.
Ushindi mashuhuri zaidi wa Akilesi ulikuwa juu ya Hektor, mtoto wa mfalme wa Troia, kama kisasi dhidi ya Hektor kwa kumuua mpenzi wake, Patroklo. p53
Iliadi yenyewe haina taarifa kuhusu kifo cha Akiles, lakini vyanzo vingine vinakubali kwamba aliuawa karibu na mwisho wa vita na Paris, ambaye alimpiga mshale wa sumu kisiginoni.
Remove ads
Kisingo cha Akiles
Hadithi za baadaye zilisimulia Akiles hakuweza kuathiriwa na silaha mwilini mwake kwa sababu mamake alimtumbukiza katika Mto Styx akiwa mtoto mchanga. Isipokuwa alimshika kisingoni wakati wa kumtumbukiza, hivyo alikuwa hapa na sehemu ya pekee ambako ngozi yake iliweza kupasuliwa. Kwa hivyo, neno "kisigino cha Akiles" (ing. Achilles heel) limekuja kumaanisha sehemu penye udhaifu hatarishi.
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads
