Visasili vya Kigiriki
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Viasili vya Kigiriki ni jumla ya visasili vya Ugiriki ya Kale, yaani ukusanyaji wa masimulizi na hadithi kuhusu vyanzo, miungu na mashujaa wao. Ilikuwa moja ya sehemu za dini ya Ugiriki ya Kale.


Chanzo kikuu kuhusu imani ya Wagiriki wa kale kabisa ni shairi la Theogonia lililotungwa na Hesiodo mnamo mwaka 700 KK.
Remove ads

Watitani ni nasaba ya kwanza ya miungu katika visasili vya Kigiriki. Kiasili ni Watitani 12, wakiwemo 6 wa kiume na 6 wa kike wanaofunga ndoa kati yao na kuzaa Watitani wengine. Mkuu wao alikuwa Kronos hadi alipopinduliwa na mwanawe Zeus aliyeanzisha nasaba ya pili ya miungu ya Olimpos. Sehemu ya Watitani walijaribu kumpinga Zeus wakafukuzwa mbinguni.
- Hyperion – mungu wa nuru na jua, aliyemzaa mungu wa jua Helios, mungu wa kike wa mwezi Selene na mungu wa kike wa mapambazuko Eos
- Iapetos – mume wa Klymene (binti wa Okeanos), aliyefukuzwa baadaye mbinguni
- Koios, aliyefukuzwa baadaye mbinguni
- Kreios – mume wa Eurybia
- Kronos – mkuu wa Watitani, baba wa Zeus, mume wa Rhea; alipinduliwa na Zeus akafukuzwa mbinguni akitawala kisiwa cha heri
- Mnemosyne – mama wa Muzi tisa
- Okeanos – mkuu wa bahari na himaya ya maji, baba wa miungu yote ya mito na pepo wa bahari na visima
- Phoibe – mke wa Koios, mungu wa mwezi
- Rhea – mama wa Hestia, Demeter, Hera, Hades, Poseidon na Zeus; alimfuata mumewe Kronos alipoondoka mbinguni
- Themis – mungu wa kike wa haki na mke wa pili wa Zeus; anajua wakati ujao
- Tethys – mke wa Okeanos
- Theia – mke wa Hyperion
Remove ads
Remove ads
Remove ads
- Hekatonkheire (Ἑκατόγχειρες) — majitu yenye mikono mia na miungu wa dhoruba na vimbunga.
- Briareo (Βριάρεως)
- Coto (Κόττος)
- Gige (Γύγης)
- Siklopsi (Κύκλωψ) - majitu-chongo watatu.
- Arge (Ἄργης)
- Bronte (Βρόντης)
- Sterope (Στερόπης)
![]() |
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Remove ads
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads