Aslay Isihaka Nassoro

mwanamuziki wa Tanzania From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Aslay Isihaka Nassoro (maarufu kama Dogo Aslay; alizaliwa 06 Mei, 1995) ni msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania.

Ukweli wa haraka Jina la kuzaliwa, Amezaliwa ...

Maisha

Aslay alikulia katika familia ya kawaida huko Dar es Salaam. Akiwa mdogo alionyesha mapenzi ya dhati kwa muziki, akiimba katika matukio ya shule na mitaani. Pia Alianza safari yake ya muziki akiwa kijana mdogo, akipata msukumo kutoka kwa wasanii wakubwa wa Tanzania waliomtangulia. Alianza kufahamika kuanzia mwaka 2011 baada ya kutoa kibao chake cha Nakusemea alichokitoa akiwa chini ya Mkubwa Fella. Kabla ya hapo, alitoa wimbo mwingine uitwao Niwe Nawe akiwa amemshirikisha Temba. Baadaye akatoa nyimbo nyingine kadhaa kabla ya kujiunga na Yamoto Band bendi ya vijana ya Yamoto Band.

Akiwa ndani ya bendi hiyo, alionesha uwezo mkubwa sana wa kuimba, akiwa na wenzake, Beka Flavour, Maromboso na Enock Bella. Nyimbo alizoshiriki kutunga na kuimba akiwa Yamoto Band ni pamoja na Yamoto (Nitajuta), Cheza Kwa Madoido, Mama, Nisambazie Raha na nyingine nyingi.

Yamoto Band haikudumu sana ambapo ilianza 2013/2014 hadi 2017 ilipovunjika kwa sababu mbalimbali na wasanii waliokuwa kwenye kundi hilo kuanza kufanya kazi zao kwa kujitegemea. Kuanzia 2017, Aslay akiwa msanii wa kujitegemea chini ya meneja wake wa zamani, Chambuso, alianza upya kung'ara.[1]

Akiwa msanii wa kujitegemea, ametoa nyimbo nyingi mfululizo hali ambayo imechanganya wengi, lakini mwenyewe alielezea kwanini amefanya ni kwa sababu hana nyimbo nyingi alizofanya akiwa msanii wa kujitegemea zaidi ya zile alizokuwa na Yamoto Band[2]

Ili asiimbe za Yamoto akiwa kwenye matamasha, kaamua kutoa nyimbo nyingi. Nyimbo hizo ni pamoja na Angekuona, Usiitie Doa akiwa na Khadija Kopa, Muhudumu, Baby, Likizo (wimbo)|Likizo, Pusha, Natamba na Huna. Awali ilitazamika kama Mkubwa Fella ndiye hasa mmiliki wa muziki wa kizazi kipya, lakini kupitia Aslay, Chambuso anasema si lazima yeye ndiye awe meneja bora wa muziki huu.[3]

Remove ads

Mafanikio na tuzo

Alichaguliwa kuwania tuzo za Kora 2012""

Ingawa Aslay ametoa nyimbo nyingi zilizopendwa na mashabiki, taarifa maalum kuhusu tuzo alizoshinda hazipatikani katika vyanzo vya sasa.

Tazama pia

  • Yamoto Band

Marejeo

Loading content...

Viungo vya nje

Loading content...
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads