Aspaja
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Aspaja ni tatizo la akili[1] linaloonyeshwa na shida katika kuwasiliana na wengine na kuanzisha uhusiano wa kijamii.
Kwa sababu hizo aspaja imewekwa katika kundi la ugonjwa wa tawahudi, neno lilotoholewa kutoka katika lugha ya Kiarabu linapomaanisha upweke, kupenda kukaa peke yake au kujitenga ikiwa ni moja ya tabia za mtu mwenye aspaja na tawahudi kwa jumla.
Watu walioathiriwa wana ugumu wa kuelewa hisia; wana uwezo wa kupata hisia kama vile pendo, lakini kwa njia tofauti.
Watu wenye ugonjwa wa aspaja [2] mara nyingi ni watu wenye akili sana. Wamejaliwa kumbukumbu ya ajabu na mantiki ndiyo msingi wa hoja zao. Pia wana ufahamu mkubwa na ujuzi mzuri wa uchambuzi.
Tunaona katika ugonjwa huu kuharibika kwa mawasiliano na wengine. Mtu aliye na dalili hii ana ugumu wa kutambua maana ya sura ya uso, maana ya sauti, na maana ya ishara za mwili za watu wengine. Ni lazima ajifunze na haichukui kiotomatiki kama watu wengine wanavyofanya. Anatumia akili na mantiki yake kubaini mambo, huku wengine wakielewa kiasili bila kufikiria.
Pamoja na watu maarufu wenye aspaja tunaweza kukutana na mfano wa Elon Musk[3].
Ugonjwa huo husababisha wasiwasi mkubwa wa ndani.
Remove ads
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads