Aust-Agder

From Wikipedia, the free encyclopedia

Aust-Agder
Remove ads

Aust-Agder ilikuwa moja kati ya Majimbo ya Norwei (fylke), ikipakana na Telemark, Rogaland, na Vest-Agder. Kunako mwaka wa 2002, kulikuwa na wakazi takriban 102,945, ambayo ni 2.2% ya jumla ya idadi ya wakazi wa nchini Norwei. ILikuwa na kilomita za mraba zupatazo 9,212 (3,557 sq mi). Kitovu cha utawala wa jimboni hapa kilikuwa mjini Arendal.

Thumb
Vegår, Aust-Agder
Thumb
Mahali pa Aust-Agder nchini Norwei

Jimbo, ambalo lilikuwa katika pwani ya Skagerrak, lilitoka Gjernestangen hadi Risør hadi Kvåsefjorden hadi Lillesand. Sehemu za ndani za maeneo yake ni pamoja na Setesdalsheiene na Austheiene. Takriban 77% ya wakazi wake walikuwa wanaishi katika eneo la pwani, ambapo ndipo kuna ujenzi mkubwa kabisa. Utalii ni muhimu mjini hapa, kama jinsi ilivyo Arendal na miji mingine ya pwani ni vivutio maarufu.

Jimbo hili lilijumuisha kisiwa cha Tromøy, Justøya, na Sandøya. Ndani ya jimbo lilijumuisha wilaya ya Setesdal, kupitia mto Otra unaomwagikia baharini.

Baada ya kuunganisha na Vest-Agder, jimbo linaitwa Agder.

Remove ads

Manispaa zake

Aust-Agder iligawanyika katika manispaa 15:

Maelezo zaidi Ukubwa, Jina ...
Remove ads

Marejeo

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads