Bahari ya Kaspi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Bahari ya Kaspi
Remove ads

Bahari ya Kaspi (Kiarabu: بحر قزوين Baḥr Qazvin; Kiajemi: دريا خزر darya khazar; Kirusi: Каспийское море kaspiiskoye more) ni ziwa kubwa kabisa duniani lenye eneo la km² 371,000 na mjao wa km³ 78,200. Liko kati ya Azerbaijan, Urusi, Kazakhstan, Turkmenistan na Irani.

Thumb
Bahari ya Kaspi kutoka angani.
Thumb
Stenka Razin (Vasily Surikov)

Kimo chake kinafikia mita 1,025.

Huitwa "bahari" kwa sababu maji yake ni ya chumvi ingawa si kali sana kama ya bahari yenyewe.

Remove ads

Maji ya chumvi

Upande wa kaskazini inaingia mito miwili mikubwa ya Volga na Ural. Inasababisha kiasi kidogo cha chumvi upande huo wa kaskazini. Asilimia ya chumvi huonegezeka kuelekea kusini.

Madini

Chini ya bahari kuna akiba kubwa za mafuta ya petroli na gesi, hasa karibu na Baku. Katika hori ya Kara-Bogas chumvi hulimwa.

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads