Barnaba Classic
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Elias Barnabas Inyasi (ambaye anajulikana kwa majina yake ya kisanii, Barnaba Classic au Barnaba Boy [1]) ni mwimbaji, mtunzi wa nyimbo na mwigizaji kutoka Tanzania.

Kazi
Barnaba alianza safari yake ya muziki mwaka 2000 kwa kupata mafunzo ya uimbaji katika kwaya ya kanisa lao la nyumbani. Baadaye aligunduliwa na kujiunga na Tanzania House of Talent (THT) akiwa na umri wa miaka 17. Wimbo uliompa umaarufu mkubwa ulikuwa Baby I Love You uliotolewa mwaka 2007.[2][3]
Mwaka 2022, alitoa albamu yenye nyimbo 19[4] ikiwashirikisha wasanii 20 kutoka Afrika Mashariki.[5]
Jarida la Music In Africa na mwandishi wa habari za muziki kutoka Tanzania, Charles Maganga, walimsifu Barnaba kwa albamu yake Love Sounds Different, wakieleza kuwa kazi hiyo yenye nyimbo 18 ndiyo kazi bora zaidi ya Barnaba Classic hadi sasa.[6]
Remove ads
Tuzo
Katika Tuzo za Muziki Tanzania (Tanzania Music Awards) za mwaka 2023, Barnaba alishinda tuzo ya Albamu Bora ya Mwaka kwa albamu yake "Love Sounds Different". Hata hivyo, aliamua kumpa Marioo tuzo hiyo kama ishara ya kuthamini kazi yake.
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads