Bobby Farrell
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Bobby Farrell (Aruba, 6 Oktoba 1949 - St. Petersburg, Urusi, 30 Desemba 2010) alikuwa mwimbaji wa kiume wa bendi ya muziki wa pop na disco-Boney M., kunako miaka ya 1970.
Farrell aliondoka mjini Aruba akiwa na umri wa miaka 15 na baada ya hapo akaja kuwa baharia. Farrel pia aliwahi kuishi nchini Norway na Uholanzi kabla ya kuhamia nchini Ujerumani. Akiwa huko, alifanya kazi nyingi akiwa kama Dj na baadaye akakutana na mtayarishaji wa muziki wa Kijerumani bwana Frank Farian na akamtaka Farrell awe mmoja wa wanakundi lake la muziki maarufu kama Boney M. Farrell akaja kuwa mwimbaji pekee wa kiume katika bendi hiyo, ingawaje, Farian baadaye alisema kwamba Bobby hakufanya kazi sehemu kubwa sana, na akasema kwa kila wanapo ingiza sauti katika nyimbo basi nayeye Farian hushriki katika rekodi hizo. Farrell alikuwa akifanya hadi matamasha ya maukumbi mbalimbali.
Kunako mwaka wa 2005 Farrell alionekana kama mchezaji katika sehmu ndogo ya video ya mwanamuziki Roger Sanchez, nyimbo ilikuwa Turn on the Music.
Remove ads
Albamu alizotoa
Nyimbo maarufu
- 1982: Polizei / A Fool In Love
- 1985: King OF Dancing / I See You
- 1987: Hoppa Hoppa / Hoppa Hoppa (Instrumental)
- 1989: Tribute To Josephine Baker
- 2004: Aruban Style (Mixes) S-Cream Featuring Bobby Farrell
- 2006: The Bump EP
Bobby Farrell na Boney M. / Boney M. Wakishirikiana na Bobby Farrell / Bobby Farrell Akishirkiana na Sandy Chambers
- 2000: The Best Of Boney M. (DVMore)
- 2001: Boney M. - I Successi (DVMore)
- 2001: The Best Of Boney M. (II) (compilation)
- 2001: The Best Of Boney M. (III) (compilation)
- 2005: Boney M. - Remix 2005 (featuring Sandy Chambers) (nyimbo mchanganyiko) (Crisler)
- 2007: Boney M. - Disco Collection (compilation)
Tafadhali elewa kwamba: Matoleo yote ya yaliyoingiliana na rekodi za vibao vya Boney M. havikuwa katika matoleo halisi ya albamu za Boney M.
Remove ads
Viungo vya Nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads