Kijerumani

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kijerumani
Remove ads

Kijerumani (kwa Kiswahili cha kale: Kidachi[1], kwa Kijerumani: Deutsch au (die) deutsche Sprache) ni lugha ya Kijerumaniki ya magharibi katika jamii ya lugha za Kihindi-Kiulaya. Huzungumzwa hasa katika nchi za Ujerumani, Austria, Uswisi, Liechtenstein na Luxemburg. Kuna pia wasemaji asilia katika nchi jirani za Ujerumani / Austria kama Ubelgiji, Uholanzi, Ufaransa, Denmark, Polandi na Italia. Nchi nyingi za Ulaya ya Mashariki zilikuwa na wasemaji wa Kijerumani lakini wengi walifukuzwa au kuondoka wakati wa Vita Kuu vya Pili vya Dunia au baadaye; vikundi vimebaki hasa katika Hungaria, Romania, Ucheki, Urusi na Kazakhstan.

Ukweli wa haraka Kijerumani Deutsch (de), Lugha ...
Thumb
Hadhi ya Kijerumani katika nchi mbalimbali.

Vikundi vidogo vya watu waliohamia katika karne za 19 na 20 wanaoendelea kutumia Kijerumani wako katika Amerika ya Kaskazini (Marekani, Kanada), Amerika Kusini (Brazil, Chile) na Afrika (hasa Namibia na Afrika Kusini).

Kijerumani huzungumzwa na watu milioni 100 katika Ulaya, ambako ni lugha ya pili kwa wingi wa wasemaji baada ya Kirusi kushinda Kifaransa na Kiingereza.

Remove ads

Lugha ya kitaifa

Kijerumani kinatumiwa kama lugha rasmi kitaifa katika nchi zifuatazo:

Lugha rasmi kieneo

Kijerumani kinatumiwa kama lugha rasmi ya utawala kieneo (ama kimkoa au kwenye ngazi ya miji / tarafa tu) katika nchi zifuatazo:

Umoja wa Ulaya

Kijerumani ni kati ya lugha rasmi za Umoja wa Ulaya pamoja na Kiingereza na Kifaransa. Ndani ya Umoja huo ndiyo lugha yenye wasemaji wengi kushinda nyingine zote.

Remove ads

Lugha inayofundishwa

Kijerumani kama lugha ya kigeni kinafundishwa shuleni au kwenye taasisi za elimu ya watu wazima katika nchi nyingi. Mwaka 2004 idadi ya wanafunzi wa Kijerumani ilikuwa kama ifuatayo:

Kijerumani ni lugha ya pili katika mtandao (intaneti) baada ya Kiingereza. Takriban nusu ya kurasa zote mtandaoni ni za Kiingereza, lakini Kijerumani kinafuata kikiwa na 8% za kurasa zote.

Kijerumani kimeathiri kwa kiasi fulani lugha ya Kiswahili cha Tanzania bara kama vile kukikopesha maneno mbalimbali, kwa mfano: shule, hela n.k.

Remove ads

Maneno machache

hujambo? – sijamboWie geht es dir? – Mir geht es gut.
jamboHallo!
ndiyoja
hapananein
mgeniGast, Fremder
rafikiFreund
karibuWillkommen!
kwa heriAuf Wiedersehen!
asanteDanke!
asante sanaVielen Dank!
safariReise
ninakupendaIch liebe dich.
hatariGefahr
daktariDoktor
polepolelangsam
Afya! (wakati wa kunywa na mwingine)Prost!
kijijiDorf
mjiStadt

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads