Bohemian Rhapsody

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Bohemian Rhapsody ni wimbo wa bendi ya Rock ya Uingereza Queen. Ilitungwa na Freddie Mercury ikatolewa kwenye albamu yao ya mwaka 1975 A Night at the Opera.

Muundo

Bohemian Rhapsody ina sehemu sita:[1]

1.Ufunguzi(0:00–0:49)– 14 %
2.Wimbo la masimulizi(0:49–2:37)– 31 %
3.Solo ya gitaa(2:37–3:03)07 %
4.Mwigo wa kubeza opera(3:03–4:08)– 18 %
5.Muziki wa rock kali(4:08–4:55)– 13 %
6.Kufunga kitulivu(4:56–5:55)– 17 %

Video

Kampuni ya EMI iliyotoa albamu ilikuwa na wasiwasi juu ya wimbo ikaona afadhali kutengeneza video ili kuongeza umaarufu wake. Wimbo pamoja na video zilifanykiwa sana na kuwa kielelezo kwa kawaida ya baadaye ya kutangaza nyimbo na bendi kwa njia ya video.[2]

Mafanikio kwenye chati

Mwanzoni kampuni ya rekodi ilikuwa na wasiwasi kama wimbo huo utapokewa kwenye vituo vya redio kwa sababu ya urefu wake (dakika 5 na sekunde 55) na muundo wake uliokuwa tata ukilinganishwa na nyimbo za siku zile[3]. Walifanya majaribio kwa kuitoa awali kwa kituo cha redio ya Capital Radio; katika wikendi moja ilisikika mara 14 na wasikilizaji walipenda sana[4]. Baadaye ikawa #1 kwenye chati nyingi. [5] Sasa inachezwa kwenye redio kwa urefu kamili.

Marejeo

Tovuti za Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads