Kichakato kikuu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kichakato kikuu (pia Kitengo kikuu cha uchakataji au KIU [1]; pia: CPU, kifupi cha Kiingereza "central processing unit") ni kichakato muhimu zaidi ndani ya tarakilishi.

Kazi yake
Ni kama ubongo wa mashine hiyo kwa sababu kila sehemu ya tarakilishi inahitajika kwa njia fulani kutekeleza shughuli zake. Kichakato kikuu huwa na saketi elektroniki inayotekeleza maagizo ya programu na kupeleka shughuli kwa sehemu nyingine za kompyuta[2].
Muundo
KIU / CPU ina sehemu tatu ambazo ni muhimu kwa utendakazi wake. Nazo zinaitwa:
- Kitengo cha Hesabu na Mantiki (KIHEMA) (Arithmetic Logic Unit (ALU))
- Kitengo cha Udhibiti (Control Unit)
- Rejesta (Processor registers)
Sehemu hizo zinaunganishwa kwenye chipu moja.[3]
Kitengo cha Hesabu na Mantiki (KIHEMA)
KIHEMA au Arithmetic Logic Unit ni sehemu muhimu ya kichakato kikuu ambayo hushughulikia vitendo vyote vya hesabu, kama vile kujumlisha, kuzidisha, kutoa, kugawanya na hesabu zote za kulinganisha. KIHEMA kina kundi la rejesta — kumbukizi ziliyojengewa moja kwa moja ndani ya KIU ili kushikilia data inayochakatwa.[4].
Kitengo cha Udhibiti
Kitengo cha Udhibiti au Control Unit inathibiti amri za programu na kuzituma kwa sehemu nyingine za KIA. Inaratibu vifaa vyote vinavyoingiza na kutoa taarifa mbalimbali katika kompyuta. Vifaa hivi vyaweza kuhusisha skrini, bao bonye, kipanya, printa, na nyinginezo nyingi.
Kumbukumbu kuu
Kwa kawaida kichakato kikuu huhitaji kiasi fulani cha kumbukumbu ambayo hurahisisha uhifadhi wa taarifa mbalimbali mara zinaposubiri nafasi ya kuweza kuwekwa katika hali ya mchakato kuziwezesha taarifa hizo kutoa matokeo yaliyokusudiwa. Sehemu hii ni ya muhimu zaidi kwani hurahisisha kazi ya kichakato kikuu na kuiwezesha kutoa matokeo yaliyokusudiwa kwa muda mfupi kwa kupunguza umbali na muda wa kuzihusisha taarifa mbalimbali wakati wa mchakato
Remove ads
Utengenezwaji
Kichakato kikuu ni kifaa muhimu na chenye gharama kubwa, hivyo utengenezwaji wake ni wa gharama kubwa. Si kila mtu ana uwezo wa kuzitengeneza, hivyo basi ni kampuni chache zenye uwezo wa kukitengeneza. Kampuni hizo zinajumisha Intel, AMD, POWERPC na nyinginezo.
Upatikanaji
Upatikanaji wa kichakato kikuu unategemea kasi, ukubwa wa mchakato wa data, pamoja na bei na unaweza kuzinunua popote pale kwenye maduka ya spea za kompyuta. Pia unahitajika kujua muingiliano wa kichakato kikuu cha kompyuta unayoitumia na spea utakayoinunua kabla hauja inunua kwani haitaweza kufanya kazi ipasavyo ikiwa kutakuwa na utofauti baina ya bodi mama na kichakato kikuu.
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads