Cheusi Mtungi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Cheusi Mtungi ni jina la uhusika kutoka katika tamthiliya ya Siri ya Mtungi kutoka nchini Tanzania. Uhusika umechezwa na Godliver Gordian. Cheusi ni mke wa Cheche Mtungi. Anapitia magumu mengi kwenye ndoa yake lakini anayatatua kwa aina yake. Sifa kuu ya Cheusi ni uvumilivu wake katika ndoa - hasa ukizingatia mumewe ni mtu wa wanawake sana. Sifa nyengine aliyonayo ni pamoja na upole na unyenyekevu kwa mume na mama yake mzazi Bi. Mwanaidi. Hapendi kuyumbishwa kwa ndoa yake na mtu yeyote yule hata kama ni mama yake mzazi ndiye myumbishaji.[1] Kwa upande wa familia aliyozaliwa, yeye ni mtoto wa kwanza wa Bi. Mwanaidi ambaye ni mke wa pili wa Mzee Kizito. Cheusi ni dada wa Shoti, ambaye anaonekana kidogo kuwa na kautahira.
Remove ads
Tazama pia
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads