Konyeza-vichanio

From Wikipedia, the free encyclopedia

Konyeza-vichanio
Remove ads

Konyeza-vichanio (kutoka Kiing. comb jelly) ni wanyama wadogo hadi wakubwa kiasi wa bahari ambao huainishwa katika faila Ctenophora (kutoka Kiyunani κτείς = kichanio, na φέρειν = kubeba). Hawakaziki kamwe lakini huogelea majini kama konyeza wengine. Na kama wanyama-upupu wote mwili wa konyeza-vichanio umeumbwa kwa tabaka la kolajini (collagen) na proteoglycans lililofunikwa na seli nje na ndani, lakini unene wa matabaka haya ya seli ni seli mbili kinyume na matabaka ya wanyama-upupu ambayo yana seli moja tu. Tabaka la nje la seli liitwa epidermi (epiderm) na tabaka la ndani liitwa gasterodermi (gastroderm). Kati ya mwili ni uwazi ulio na kipenyo kikubwa kiasi juu (“mdomo”) na vipenyo vidogo viwili chini (“mikundu”). Kipande cha juu cha uwazi huu ni kama koromeo na mdomo wake unaweza kufungwa. Kipande cha chini ni kama tumbo. Takriban spishi zote zina safu nane za “vichanio” vilivyoumbwa kwa vijisinga vingi ambavyo vinapiga chini ili kusukuma mnyama mbele (asili ya jina lao). Spishi nyingi zina minyiri miwili inayotumika kwa kukamata mawindo kwa msaada wa seli za kunata (colloblasts).

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Thumb
Muundo wa konyeza-vichanio; nyekundu: koromeo; kijani: mnyiri; njano: ala ya mnyiri; kijivu: mesoglea; ///: vichanio
Remove ads

Picha

Makala hii kuhusu "Konyeza-vichanio" inatumia neno (au maneno) ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio la kutafsiri neno (au maneno) la asili comb jelly kutoka lugha ya Kiingereza. Neno (au maneno) la jaribio ni konyeza-vichanio.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.

Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads